Posts

Showing posts from June, 2025

Tunaye Roho - Anatuombea Lyrics sung by Acacia Singers

Tunaye Roho - Anatuombea Lyrics sung by Acacia Singers 1. Tunaye roho wake Mungu, Ambaye ni msaidizi Hutuongoza kwenye ukweli, Hata tusitende uovu Roho wa Mungu tuliyepewa, Hutukumbusha maagizo Roho wa Mungu tuliyepewa, Hutukumbusha maagizo Refrain (Na bado) Anatuombea, Juu mbinguni (Na bado) Anatuombea Dhambi zetu zipate kufutika 2. Tunaye mwana Yesu Kristo, Anatuombea kwa Baba Hutuongoza kwenye kweli, Mchunga mwema wa kondoo Mwombezi wetu kule mbinguni, Mtetezi wa wenye dhambi Mwombezi wetu kule mbinguni, Mtetezi wa wenye dhambi 3. Lishike neno lake Mungu, Ukadumu kwenye sala Naye roho mtakatifu, Atakujaza nguvu tele Roho wa Mungu tuliyepewa, Usimuache aende zake Roho wa Mungu uliyepewa, Usimuache aende zake 4. (Solo) Mpatanishi, Yesu Kristo, Yeye aliye na mauwa Kuhani wetu mwenye haki, Mtakatifu wake Bwana Mwanakondoo aliyechinjwa, Kwa ajili ya wenye dhambi Mwanakondoo aliyechinjwa, Kwa ajili ya wenye dhambi Refrain (Oh, Na bado) Anatuombea (Kule kwa Baba) Juu mbinguni (Kweli bado) ...

Ewe Bwana Nenda Nasi Lyrics sung by Osingo Secondary

Ewe Bwana Nenda Nasi Lyrics sung by Osingo Secondary Refrain Ewe Bwana nenda nasi *2 Ooh Tupe nguvu za kushinda majaribu za dunia Japo ni magumu kwetu japo ni makali Mungu wetu nenda nasi tuweze kuyashinda 1. Watoto wake Ayubu kufariki nayo Maradhi kajawa mwili mwake Mali kuhisha Ayubu hakukata tamaa Kuamini Mungu mali kurudishwa mara mbili 2. Umweleze Yesu shida zako Kimbilio yetu maishani mwako  Atatuongoza hadi tufike kwetu mbinguni Atatuongoza hadi tufike kwetu mbinguni. Songs from Home As sung by Osingo Secondary.

Nitasimulia Kisa Cha Yesu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Nitasimulia Kisa Cha Yesu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Nitasimulia kisa cha Yesu, Kwa matendo makuu aliyotenda Kwa rehema zake nitasimulia, Amebadilisha maisha yangu Sasa natambua kwamba anipenda, Nitasimulia habari zake Kamwe sitaacha kunena habari, Habari za Yesu tamu kwangu Pre-Chorus Nitasimulia habari zake, Amebadilisha maisha yangu Nilikuwa vile leo niko hivi, Amebadilisha maisha yangu Nitasimulia habari zake Chorus Mashariki (wote) kusini, wasikie Kaskazini (wote) magharibi, wasikie (wasikie) Vilindini (wote) na bahari, wasikie Juu angani viumbe viseme ya kwamba Yesu; Mfalme wa utukufu 2. Katika tanuru amenilinda, Tunduni mwa simba kashuka kwangu Amenikingia mauti juu yangu, Hukumu ya kifo aliibeba Sasa natambua kwamba anipenda, Nitasimulia habari zake Kamwe sitaacha kunena habari, Habari za Yesu tamu kwangu. Kurasini SDA Choir. For Revision; Vilindini (wote) na bahari, wasikie

Yote Yatapita Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Yote Yatapita Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Yote yatapita tuonayo, Yote yatapita tuyapendayo Kitakacho dumu ni uzima, Uzima ule wa milele Refrain Ni kitu gani kitacho dumu kwako Ulivyonavyo vyote ni ubatili Vyote vyatoweka havidumu, Tafuta uzima milele 2. Mali utajiri vyatoweka, Maisha ya sasa yanatoweka Yesu analeta maisha mapya, Yote ya kale yanapita Outro Mambo yote yanapita yatoweka Tarajia uzima wa milele Nasema, kaza mwendo usichoke Yesu aleta mambo mapya. Kurasini SDA Choir.

Ninayaweza Mambo Yote Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Ninayaweza Mambo Yote Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Ninayaweza mambo yote, Kwa jina la Yesu Nimejifunza kumtumaini siku zote Refrain Nayaweza yote kwa jina la Yesu, Mbele yangu (ni)naona nuru Anaongoza mapito yangu, Ni jibu kwa mashaka yangu Sitapungukiwa chochote, Anajua shida zangu 2. Furaha amani ninatapata, Kwa jina hili Ni mtetezi wangu nikiitwa hukumuni. Kurasini SDA Choir.

Kiasi Gani - Rudi Nyumbani Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Kiasi Gani - Rudi Nyumbani Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Kiasi gani watanga mbali na Bwana Na umerushwa rushwa huku na kule Dunia imejaa mahangaiko, Mahangaiko taabu za maisha Rudi nyumbani, rudi kwa Bwana Unahangaika bure, rudi nyumbani Refrain Rudi nyumbani, rudi kwa Bwana, Sasa yatosha, rudi nyumbani Kuna mambo mazuri yanayokungojea, Kivulini mwa Yesu kuna faraja, Nyumba ni nyumbani utakuwa hura Kuna sauti inakuita, Rudi nyumbani Bwana anakuita 2. Duniani kuna mbwa mwitu wakali Wasio na huruma wala hisani Waliotayari kukuangamiza Watakurarua wakuangamize Rudi nyumbani, mwanangu rudi Unahangaika bure, rudi nyumbani. Kurasini SDA Choir.

Safari Ya Mbinguni Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Safari Ya Mbinguni Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Safari ya mbinguni; Kwenye njia nyembamba Tumaini linapotoweka Nainua uso wangu Nitazame juu, Sing ladies; Ninapaza sauti; ‘Yesu uniokea’ Refrain Eeeeh; Katika mikono ya Bwana nimetia nanga, Oooh; Katika shida nilimwita akanisikia Mikononi mwa Bwana kivuli cha faraja, ‘Enyi nyote mliolemewa,’ Bwana, anawaita 2. Katika giza hili; Yesu aliniona Akayafuta machozi yangu Nikawa mtumwa huru Nina amani, Sing ladies; Bila Yesu ni bure, Sasa nina amani. Kurasini SDA Choir.

Kama Kwenye Ngazi - Mungu Akiwa Upande Wetu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Kama Kwenye Ngazi - Mungu Akiwa Upande Wetu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Kama kwenye ngazi ya Yakobo, Malaika walifurika Wengi washuka, wengi wapanda Wakimzunguka, (Zunguka!) Wengi washuka, wengi wapanda Wakimzunguka, (Zunguka!) Pre-Chorus Mungu akiwa upande wetu, Ni nani wa kutuogofwa? Hutuzunguka hutuinua Mikononi mwake Chorus Ni kama mlima wa Zayuni -(Kama mlima---wa Zayuni) Hutuzunguka kote kote -(Huzunguka---kote kote) Najivunia jina lenye nguvu -(Najivuna jina---lenye nguvu) Nimetulia, tena nina nguvu -(Natulia tena---nina nguvu) Mungu akiwa upande wetu tumogope nani? Mungu akiwa upande wetu tumogope nani? 2. Kama kwenye ngazi ya Yakobo, Ngazi yangu hulindwa naye Sina mwingine, Sina mwingine, Yesu anitosha, (Atosha!) Sina mwingine, Sina mwingine, Yesu anitosha. Kurasini SDA Choir.

Asikutaabishe Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Asikutaabishe Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1 Asikutaabishe maana yeye haendi Asikutaabishe safarini hayupo Safari ya kwenda mbinguni Ni ya mtu mwenyewe Asikutaabishe, Umtazame Yesu Refrain Hayupo, hayupo safarini hayupo Yesu arudipo mwovu hana nafasi Asikuguze Shetani Mwisho wa safari 2. Majina yaitwapo jina lake halipo Alishahukumiwa sababu ya uasi Hana nafasi juu mbinguni Asikutaabishe Safari ya mbinguni, Umtazame Yesu. Kurasini SDA Choir.

Bwana Umenichunguza Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Bwana Umenichunguza Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Bwana umenichunguza kote kote Na we’ umenijua hata kuketi kwangu Na we’ wajua matendo yangu yote Nikufiche nini Bwana wangu Refrain Hata nikijificha katika pango la giza (nene), bado ni kazi bure Kwa mkono hodari utanitafuta huko, kila mahali uko Njia zako za ajabu hazichunguziki, hazichunguziki Mimi ni kiumbe wewe ni muumba Hata nikilala chini ya bahari Njia zangu zote waziijua Ninajidanganya naja kwako Bwana 2. Tunajifunza somo hili kwa Yona Alipotaka kwenda kujificha Tarshishi Bila kujua akakutana nawe Alipotoroka uso wako. Kurasini SDA Choir.

Kati Ya Waloachwa Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Kati Ya Waloachwa Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Kati ya wal’oachwa humu Kati ya wal’opewa msamaha Na mimi nilikuwa mmoja wao Na mimi, Nasema; na mimi Nikapewa msamaha Refrain Nikajiuliza kwa nini mimi? (kwa ni---‘mi-mi’4) Mimi, kwa nini mimi? Neema za Mungu ziwe juu yangu Ni upendo wa ajabu 2. Gereza likafunguliwa Wafungwa tuka-achwa huru Na wote tukatoka gerezani Na wewe, Nasema; na mimi Nikapata msamaha. Kurasini SDA Choir. Waloachwa; Wal’oachwa; Walioachwa

Nani Kati Yenu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Nani Kati Yenu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Nani kati yenu mtoto akimwomba mkate, Yeye kama mzazi---atampa jiwe? (Hum*3) Nani kati yenu mtoto akimwomba samaki, Yeye kama mzazi---atampa nyoka? (Hum*3) Baba wa mbinguni ni Baba anayetupenda Mahitaji yetu---ajua ya kesho (Hum*3) Anasema bisha malango ya mbinguni wazi, Kila abishaye---atafunguliwa Pre Chorus Ameahidi baraka tele, Na ahadi zake ni za kweli Msiwaze mambo ya kesho, yeye ayajua Njooni kwake kwa ujasiri, Na enyi nyote mliolemewa Msiwaze mambo ya kesho, yeye ayajua Chorus Tunajivunia Yesu, nani kama wewe? Baba anayejua kutunza, analea Mahitaji yetu yote mikononi mwake, Hakika, (na) atupenda Ni lini ‘tafika kwake nimwone uso kwa uso? Yesu (Yesu), atupendaaa… 2. Ninajivunia jina la Yesu la thamani, Kwake ninapata---uzima milele (Hum*3) Ninajivunia simba wa kabila la Yuda, Kivulini mwake---napata faraja (Hum*3) Kila nikimwita yu tayari kunisikia, Yuko ndani yangu---nami ndani yake (Hum*3) Anasema bisha malango ya mbinguni wa...

Kitu Gani Kitachokutenganisha - Chagua Hivi Leo Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Kitu Gani Kitachokutenganisha - Chagua Hivi Leo Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Kitu gani kitachokutenganisha, Na upendo wa Yesu ukajitenga naye Tangu umjue Mwokozi wako, Amekuwa ngao kimbilio Refrain Chagua chagua hivi leo ni nani utakayemtumikia Utasita kati ya njia mbili hatarini (wewe) Chagua utakayemtumikia Chagua chagua, chagua chagua, Chagua chagua, utakayemtumikia Lakini mimi, mimi na nyumba yangu tutamtumikia Mungu wetu Lakini mimi, mimi na nyumba yangu tutamtumikia Mungu wetu 2. Ni wakati wa kufanya uamuzi, Acha kutangatanga kati ya njia mbili Msimamo wako una mashaka, Utangatanga hata lini? Kurasini SDA Choir.

Fungua Fahamu Zangu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Fungua Fahamu Zangu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Fungua fahamu zangu Bwana, Nitaambue maagizo yako Fahamu zangu ni mali yako, Fungua fahamu zangu nione Fahamu zangu ni mali yako, Fungua fahamu zangu nione Refrain Mimi ni mali yako, Wewe u mali yangu Fungua fahamu za moyo wangu, Nikuone Yesu ndani yangu Nikumbushe nisiache agizo, Nisimame katika neno lako (neno lako) 2. Fungua fahamu zangu Bwana, Niitambue sauti yako Niwe mtiifu (na) mnyenyekevu, Fungua fahamu zangu nione Niwe mtiifu (na) mnyenyekevu, Fungua fahamu zangu nione. Kurasini SDA Choir.

Umeshupalia Kibanzi - Toa Boriti Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Umeshupalia Kibanzi - Toa Boriti Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Umeshupalia kibanzi kwenye jicho la nduguyo Fanya matengenezo msaidie Sote tumepungukiwa na utukufu wake Mungu Ebu fanya matengenezo Refrain Toa boriti kwenye jicho lako kwanza Ukamsaidia nduguyo Sote tu wasafiri Kwenda Kanaani Sote twarejea kwa Mwokozi 2. Umekuwa hakimu wa kuhukumu dhambi za nduguyo Fanya matengenezo msaidie Ndugu yako akikosa njia muonye kwa upole Ebu fanya matengenezo. Kurasini SDA Choir. Shupalia - To affirm with urgency, To Insist. Definition Source; https://swahili-dictionary.com/swahili-english/shupalia_shupalia

Tulipofika Kila - Kila Goti Litapigwa - Wastahili Heshima Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Tulipofika - Kila Goti Litapigwa - Wastahili Heshima Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Tulipofika kwenye miamba ya kutisha, Yesu akawa ni mwamba wa kale Tulipovuka bahari (bahari), Yesu maji ya uzima Kwenye wanyama wakali (wakali), Kaitwa simba wa Yuda Alipofika kwa wenye wadhambi, Wakamwita Imanueli Mungu pamoja nasi Refrain Kila goti litapigwa litapigwa Hakika mchana kweupe Kila ndimi litakiri likisema, Wazi wewe mwana wa Mungu Wastahili heshima leo, Hata milele milele 2. Tutakapofika mbinguni tutamuona, Itakuwa ni furaha ajabu Kufumba na kufumbua (fumbua), Makovu yataponyeshwa Majeruhi watapona ('tapona), Hakuna maombolezo Tutakapofika kwenye meza ya fahari, Imanueli atakuwa wa kwanza. Kurasini SDA Choir.

Inueni Mioyo/Roho Mtakatifu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Inueni Mioyo/Roho Mtakatifu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Inueni mioyo mtazame juu  Pokeeni roho mtakatifu Ndiye msaada wetu mfariji Inueni mioyo mtazame juu Refrain Kiongozi amini kwa wakati Fungue mioyo yenu mjazwe roho Ndiye roho wa kweli si wa machafuko Atawaongoza awape amani Njoo roho mtakatifu utushike mkono 2. Roho mtakatifu ni msaada Hupatikanao kwa wakati Fungueni mioyo aingie Roho mtakatifu njoo kwangu. Kurasini SDA Choir.

Tazama Upendo - Mikoni Mwa Yesu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Tazama Upendo - Mikoni Mwa Yesu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Tazama upendo wa Mwokozi Yesu Alivyotupenda hapo mwanzoni Ahitaji wote watangao mbali Wamrudie Mungu waokolewe Atafuta waliokata tamaa Waliochoshwa na dhambi Yesu anawaita Waliolemewa na mizigo moyoni Watakuwa huru atawapumzisha Refrain Hata sasa amini (wote) uwe huru Tazama utazame Kalwari Wanaomtumaini watabarikiwa Ufalme u tayari kwa ajili yao 2. Mungu wa mbinguni awapenda wote Ni mchunga mwema wakati wote Ujapopita bondeni mwa mauti Atakulinda ubaki salama Miguuni pa Yesu kuna amani Mbele yangu kuna ulinzi ulio imara Awaita wote waje waokolewe Watapata raha atawapumzisha Outro Wito wa Yesu kwa wote waliolemewa Mikononi mwa Yesu watakuwa huru Mikononi mwa Yesu, (Mikononi mwa Yesu) Waliao watafutwa machozi, njoo kwa Yesu. Kurasini SDA Choir.

Fungueni Malango Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Fungueni Malango Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Fungueni malango ya mbingu Leo ni siku ya furaha tulioingoja Ni siku kuu ya wateule toka kila pembe Nisikie furaha Marafiki waliotengana kufumba na kufumbua Watakutana tena Safari hii hakuna kifo wala kutengana Nisikie furaha Refrain Watu wataruka wataruka kama ndama Furaha! Furaha! Furaha! Ni furaha Wakizunguka zunguka kiti cha enzi Wameshinda mauti Mungu ataketi kati ya wageni wake Siku yenye iko karibu 2. Shangwe tele na vigelegele Vitasikika kutoka vinywa vya wateule Wakiimba wimbo wa Musa na Mwanakondoo Itakuwa furaha Yaliyopita yameshapita Hakuna sababu kukumbuka yaliyopita Twatazamia mambo mapya na maisha mapya Itakuwa furaha. Kurasini SDA Choir.

Wanaisraeli - Una Nini Mkononi Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Wanaisraeli - Una Nini Mkononi Lyrics sung by Kurasini SDA Choir Chorus Wanaisraeli wamekwama jangwani Wameyasahau maajabu ya Mungu 'Musa una nini mkononi? Piga mwamba watu wapate maji' Jeshi la Farao linakuja Nyosha fimbo yako juu ya bahari Wakashuhudia maajabu ya Mungu Wakapita kati ya bahari Verse 1 Bahari ikagawanyika maajabu ya Mungu  (Hum! Hum! Hum! Hum!...aaahaa) Wakapita kuvuka kati ya maji ya bahari  (Hum! Hum! Hum! Hum!...aaahaa) Na jeshi ya Farao walipofika wakazama  (Hum! Hum! Hum! Hum!...aaahaa) Wakashangilia wakamsifu Mungu Maajabu ya Mungu Chorus Wanaisraeli wamekwama jangwani Wameyasahau maajabu ya Mungu 'Musa una nini mkononi? Piga mwamba watu wapate maji' Jeshi la Farao linakuja Nyosha fimbo yako juu ya bahari Wakashuhudia maajabu ya Mungu Wakapita kati ya bahari Verse 2 Nasi leo kama wanaisraeli wasafiri  (Hum! Hum! Hum! Hum!...aaahaa) Tumetangatanga jangwani tumekosa imani  (Hum! Hum! Hum! Hum!...aaahaa) Amini! Amini! Amini! Bwana atatimiza ...

Tunataka Kumuona Yesu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Tunataka Kumuona Yesu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. 'Tunataka kumuona Yesu, Yesu Eh, Bwana tunataka kumuona Yesu Sisi tunataka kumwona Yesu,' Walikuwa wayunani Miongoni mwa waliopanda kwenda kuabudu Walimwendea Filipo wakisema; Refrain 'Bwana, Eh Bwana tunataka kumwona Yesu, Tumesikia habari zake, Tunataka kumuona Yesu, Ooh, Bwana, Eh Bwana tunataka kumuona Yesu,' Walimwomba Filipo naye akawasikia 2. Mara ngapi wewe umeomba kumwona Yesu Ili aseme na wewe, Akupe chakula cha mbingu Waweka moyo wako mbali Wafunga milango ya moyo Fungua leo, uwe kama wale (kama wale) wayunani wa kale Waliamua kumwomba Filipo kwa moyo Outro Bwana Yesu kafungua milango ya mbingu Ameinyosha mikono yake Angoja uitike ukichukua hatua kumuita Mwite leo akungoja... Atakusikiliza... Kurasini SDA Choir.

Gharama Ya Wito Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Gharama Ya Wito Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Gharama ya wito wa Yesu, Je waitambua? Alikwisha itamka mapema Uza vyote gawa vyote kisha unifuate Tutapataje kupona tusipojali? Sikia! Sikia! Sauti, Sikia! Inayokuita leo Dunia na yote yanapita yanatoweka Tutapataje kupona tusipojali? 2. Tambua sauti ya Yesu inayokuita Ya nyuma usifikiri njoo leo Moyoni kata shauri la kufuata Yesu Tutapataje kupona tusipojali? Kurasini SDA Choir.

Karibu Tutaona Jiji Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Karibu Tutaona Jiji Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Karibu tutaona jiji tulioahidiwa Msifadhaike mioyoni mwenu Yesu alitamka Jicho halijapata kuona mazuri ya mbinguni Kaza mwendo tuingie pale (pale) katika jiji. Refrain Ni shangwe shangwe vigelegele Yesu akiongoza Nuru yake yaongoza kuingia kwenye jiji Itakuwa jubilii ni shangwe juu mbinguni Ndugu kaza mwendo tuingie (pale) katika jiji 2. Barabara za kwenye jiji zimejaa dhahabu Ni kunyatanyata mwendo wa pole, mwendo wa maharusi Wakaaji wa jiji lile wamejawa na upendo Wenye chuki hawatakuwepo (pale) katika jiji. Kurasini SDA Choir.

Tulia Kwa Yesu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Tulia Kwa Yesu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Tulia kwa Yesu usitoke kamwe Teseka naye ufikie mwisho Ukazikwe na Yesu, Ufufuke naye Ndiye msaada wako, Alpha na Omega Tulia kwake usitoke Refrain Tulia kwa Bwana, Usitoke kamwe Tulia! Tulia! Tulia! Tu Usitoke kamwe uwe salama Tulia, Usitoke kamwe 2. Tufani zivume usitoke kamwe Ngome imara nyakati za taabu Muite ataitika kwenye taabu zako Yesu ndiye jibu Ni mwanzo na mwisho Tulia kwake usitoke. Kurasini SDA Choir.

Nashangaa - Kina Cha Pendo Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Nashangaa - Kina Cha Pendo Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Nashangaa nashangaa, Kina cha upendo wa Mungu wanizunguka Nashangaa tena nashangaa, Alivyo mwema kwangu siku zote Kwa mapana marefu ya pendo, Nauona waziwazi Pande zote amenizunguka, Naburudika kwenye pendo lako Natembea bila wasiwasi, Katika pendo la Yesu Refrain Kina cha pendo la Yesu, Chazidi kina cha bahari Hangaiko la machozi, Kwa Yesu ni furaha Subiri ngoja uone Yesu, Atatenda kwa wakati Kina cha upendo wa Yesu, Ni pendo lisilo kipimo 2. Nashangaa nashangaa, Maajabu ya pendo lake yanishangaza Wema wake unadumu kwangu,Pendo lake linazidi kipimo Nimeona marafiki wengi, Sijaona kama Yesu Marafiki wa dunia hii, Wamejawa na pendo la herosi Yesu ndiye rafiki wa kweli, Pendo lake linadumu. Kurasini SDA Choir.

Kisha Nikaona Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Kisha Nikaona Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Kisha nikaona mbingu nchi mpya Ikishuka hapo juu angani Jeshi la malaika wanapiga vinumbi Wakimleta Bwana harusi Refrain Kisha nikaona jiji Jerusalemi Umepambwa unameta mji ni mzuri Na wenyeji wake wapendeza Si mbali kaza mwendo ufike pale 2. Sauti za tarumbeta zasikika Ni ishara Yesu anarudi Jeshi la malaika likishuka angani Wakimleta Bwana harusi. Kurasini SDA Choir.

Ni Habari Njema Kwangu - Neema Iliyoshuka Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Ni Habari Njema Kwangu - Neema Iliyoshuka Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Ni habari njema kwangu, Ni habari njema kwangu, Habari njema kwako, Sikiliza kwa makini Neema ni bure ni bure Ilitolewa kwa wote, Ilitolewa kwa wote Tulipotanga mbali, Kama kondoo bila mchunga Kwa neema yake akatuokoa Refrain Neema iliyoshuka, Ilisafisha njia ya wokovu Ilitolewa na Mungu Baba, Kwa wenye dhambi Neema ya bure juu yangu, Neema ya bure juu yako Ilitolewa kwa ajili yangu, Na ilitolewa kwa ajili yako Pokea neema bure, Toka kwa Mungu Baba  2. Yesu alilipa bei, Yesu alilipa bei Neema bure kwangu, Niliyestahili kifo Kabeba msalaba wangu Anachohitaji kwangu, Anachohitaji kwangu Nimpe moyo wangu, Apate nafasi ndani yangu Kwa neema yake ataniokoa. Kurasini SDA Choir.

Muumbaji Mfalme Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Muumbaji Mfalme Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Muumbaji mfalme vitu vyote vyako, Moyo wangu ni mali yako Ndani yangu weka neno la uzima, Nisimame kwenye neno lako Refrain Nisimame kwenye neno, Nitangaze sifa zako Bwana Kwenye giza onyesha nuru, Kati ya mataifa Watu wakuone fungua njia, Kaa nami Bwana 2. Nipe ujasiri mwingi nisimame, Ndani yangu fanya kituo Nisimame kama mitume wa kale, Unifiche kwenye mbawa zako. Kurasini SDA Choir.

Umepimwa Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Umepimwa Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Umepimwa kwenye mizani Mizani ya Bwana Na umeonekana ndugu umepungua Mizani ya Bwana umeonekana Ya kwamba umepungua, Haleluya! Refrain Fanya matengenezo haraka Umepimwa kwenye mizani Mizani ya Bwana Umeonekana ndugu umepungua Tafakari ndugu mwenendo wako, Haleluya! 2. Ajidhaniye amesimama ataanguka Mizani ya Bwana itasimama daima Ikisema kweli kwa matendo yako Dhambi zitawekwa wazi, Haleluya! Kurasini SDA Choir.

Nimesikia Wito Wako Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Nimesikia Wito Wako Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Nimesikia wito wako, Nami sitaghairi kuja kwako Nimetambua kosa langu, Bado una makusudi juu yangu Nimetambua kosa langu, La kutanga mbali na uso wako Refrain Ulisema tukibisha tutafunguliwa, Na mimi leo ninabisha kwako Nifungulie lango la rehema, Najuta nimepoteza wakati Nimetanga mbali na we’, Sasa yatosha najuta nisamehe Wewe ni Bwana mwingi wa rehema, Nifungulie lango la rehema 2. Niite nikaseme nawe, Nikueleze haja za moyoni Ninatubu maovu yangu, Kilio changu nikusamehewa Nitamke kwa lugha gani, Nimechafuka najuta nipokee. Kurasini SDA Choir.

Sogea Karibu Nami Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Sogea Karibu Nami Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Sogea karibu nami Bwana Unikumbushe mapito yako Mimi ni dhaifu nasahau Unikumbushe uwe karibu Refrain Ninaanguka ninasimama Kama mtoto mchanga nakosa nguvu Sogea karibu unishike mkono Nina haja nawe kila saa 2. Uwe kando yangu safarini Msaada wangu ni katika Bwana Mimi ni dhaifu nasahau Unikumbushe uwe karibu. Kurasini SDA Choir.

Sielewi Ni Kwa Nini Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Sielewi Ni Kwa Nini Lyrics sung by Kurasini SDA Choir Refrain Sielewi, Sielewi ni kwa nini, Kila siku majaribu juu yangu Leo nikisema ninatubu Kesho ninarudi palepale Ni -? hili kesho nina lile, Nahitaji msaada toka juu Nimechoka natamani nipumzike, Roho iko radhi mwili ni dhaifu 1. Nagundua ni Shetani Shetani hajalala usingizi Kama simba awindaye Ndivyo anavyoniwinda Ninafika mbali kuwaza Kwamba Yesu ameshaniacha – Oooh; Kwani ninaposimama, Ndipo ninapoanguka (Sielewi!) 2. Napata faraja ninapotambua kwamba Yesu yuko nami Hajalala usingizi Ndipo ninapata nguvu Na katika hayo ndipo natambua kwamba Yesu anipenda – Oooh; Nami ninapoanguka, Yesu ananiinua (Sielewi!) Sielewi! Sielewi! Ni kwa nini? Kurasini SDA Choir. -?; Shinda, Ni ishi na Revise the Rhythm For Revision #ForRevision

Nina Rafiki Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Nina Rafiki Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Nina rafiki wa maisha, Asiyechoshwa nami Amechukua shida zangu, Anipenda upeo Refrain Ananipenda, Nampenda! Ooh Ooh Yesu, Mkombozi wangu Aliacha enzi yake, Akaja kanikomboa Mkombozi wangu, Akashuka kwangu Toka utumwani, Kaniweka huru 2. Kifo kaburi havivumi, Najua iko siku Hata nikifa, atafufuka* Yesu anaporudi Kurasini SDA Choir. Hata nikifa, *(atafufuka); (atanifufua) For Revision #ForRevision

Bwana Ameahidi - Mikaeli Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Bwana Ameahidi - Mikaeli Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Bwana ameahidi kuonyesha njia pasipo njia Akutane na shida zako akupe heri Atatengeneza njia pasipo njia waja wapite Ndiye Mungu wa yale yasiyowezekana Refrain Ataonyesha njia kwako katikati ya giza nene Kati ya tanuru la moto liwakalo Mikaeli atasimama upande wako utashinda 2. Ni Mungu anayetamka na ikawa amini leo Fadhili na neema yake iwe juu yako Akuinulie uso wake popote akurehemu Ndiye Mungu wa yale yasiyowezekana. Kurasini SDA Choir. Theme: Confidence In Chaos/Trust.

Njooni Kwenye Kisima Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Njooni Kwenye Kisima Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Njooni kwenye kisima cha Bwana, Kuna maji ya uzima tele Nyote mliojawa na kiu, Njooni kwenye kisima cha Bwana Atakayekunywa maji ya kisima, Kisima cha Mwokozi Hataona kiu milele milele Refrain Usikiapo sauti ya Bwana, Fanya hima uje leo kwenye kisima Upate maji ya uzima bure bure-bure, Yanayotolewa na Yesu bure Na wale wanaotaka kuoga, Watakuwa wasafi wana wa Mungu Njooni nyote katika kisima, Muoge na kunywa bure 2. Wito wa Yesu ni kwa watu wote, ‘Njooni kwangu mliochoka Na mliolemewa na dhambi, Nira yangu ni laini njooni Tena mzigo wangu kwenu ni mwepesi, Njooni mpumzike Nitakuwa nanyi mwisho wa dahari.’ Kurasini SDA Choir.

Fuata Nyayo Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Fuata Nyayo Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Fuata nyayo za Mwokozi kule Gethsemani Utakuta alama alipo omba Na jasho likawa damu Yesu akiomba Fuata nyayo za Mwokozi kule Gethsemani Refrain Nyayo za Mwokozi zaongoza uzimani Matone ya damu yaliyomwagika Yesu anaomba usipotee Fuata nyayo zake Gethsemani 2. Fuata nyayo za Mwokozi mlimani Golgotha Utakuta alama za misumari Elekea kaburini utaona jiwe Limekwisha ondolewa Yesu kafufuka. Kurasini SDA Choir.

Sitaionea Haya Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Sitaionea Haya Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Sitaionea haya injili ya Yesu, Kwa maana ni uweza wake Mungu Uweza unaoleta wokovu, Kwa yeye anayeamini Maana waliosikia wito ni wengi, Ni nani aliyetayari? Wote walotayari waende kwa imani, Uweza uwe juu wao Refrain Injili kwanza ajenda ya moyoni, Uweza unaoleta wokovu Kwanza wajue habari njema, Mambo mengine muachie Mungu Najua vikwazo vinavyokuja, Vitazidi kuniimarisha 2. Utayasikia mambo mengi utazame mbele, Majeraha yake ni ya kitambo Hakuna kitu kitamshinda Yesu, Ukiwa mikononi mwake Shetani hawezi kumshinda simba wa Yuda, Kumbuka pigo la jangwani Wote walotayari waende kwa imani, Uweza uwe juu yao. Kurasini SDA Choir.